TAARIFA KWA UMMA
UZINDUZI WA KOZI YA MTANDAONI YA MAFUNZO YA SWALA (SELF-PACED)

Moyo Islamic Academy inafuraha kutangaza uzinduzi wa kozi mpya ya mtandaoni ya mafunzo ya Swala inayowawezesha washiriki kujifunza kwa wakati wao wenyewe (self-paced), popote walipo.
Kozi hii imelenga kuwasaidia Waislamu kujifunza na kuboresha utekelezaji sahihi wa Swala kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu.
Kupitia kozi hii, utajifunza:
- Umuhimu wa Swala katika maisha ya Muislamu
- Namna sahihi ya kuswali hatua kwa hatua
- Masharti, nguzo na sunna za Swala
- Makosa ya kawaida katika Swala na jinsi ya kuyaepuka
Faida za kozi hii:
- Kozi hii ni BURE (baada ya kulipa ada ya maombi ambayo ni TZS 10,000 kwa Watanzania na usajili ambayo ni TZS 25,000 kwa Watanzania. i.e. Jumla ni TZS 35,000)
- Kujifunza mtandaoni popote ulipo
- Kujifunza kwa ratiba yako mwenyewe (self-paced)
- Inapatikana kupitia simu au kompyuta
- Mafunzo ya video yaliyoeleweka kirahisi
- Kwa lugha ya Kiswahili
- Cheti kitatolewa kwa atakaehitaji (Baada ya kulipia cheti na kufanya mtihani wa kujipima. Gharama za cheti/Usafirishaji popote duniani ni TZS 50,000)
Nani anaweza kushiriki?
Kozi hii iko wazi kwa Waislamu wote—wanaoanza kujifunza na wanaotaka kuboresha Swala zao.
Jinsi ya kujiandikisha:
Tembelea: Bofya hapa kujisajili
WhatsApp: 0766061270
Tunawakaribisha wote kunufaika na fursa hii ya kujifunza ibada ya msingi kwa urahisi zaidi.
Imetolewa na:
Moyo Islamic Academy (MIA)
05/05/2026
