Page 1 of 1

Child Online Protection

Posted: Tue Mar 24, 2026 10:56 am
by webmaster
Ukuaji wa teknolojia umerahisisha matumizi ya vifaa vya kielektroniki vilivyo unganishwa na intaneti kama vile simu za mkononi na kompyuta hivyo kuchochea ongezeko la watumiaji wengi ikiwemo watoto. Katika zama hizi za kidigitali ni muhimu kwa watoto kuwa na elimu ya matumizi sahihi na salama ya mtandao ili kuepuka kuwa wahanga wa matukio ya uhalifu mtandaoni.
Changamoto Mtandaoni

Endapo watoto watatumia mitandao bila usimamizi wa wazazi au walezi wanaweza kukutana na changamoto zifuatazo;
1. Kuwasiliana na watu wasiofaa

Wahalifu mtandaoni: ambao hutumia njia za ulaghai kuwashaw- ishi watoto kutoa taarifa nyeti kuhusu wao wenyenye au wazazi wao.
Wanyanyasaji wa mtandaoni (Cyberbullies):ambao mara nyingi huwa na malengo ya kuwanyanyasa watoto kisaikolojia na kuwasaba- bishia hofu au msongo wa mawazo.
Mafataki wa mtandaoni (Online Sexual Predators):ambao malengo yao ni kuwarubuni Watoto kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi

2. Kukumbana na maudhui yasiyofaa kama vile:

Maudhui ya ngono na picha za utupu.
Matukio ya kihalifu na biashara haramu.
Habari potofu.

3. Kupakua programu hatarishi au virusi vya kompyuta (malware) kupitia tovuti hatarishi, kubofya viunganishi hatarishi na pia kufungua viambatisho vya barua-pepe vyenye virusi vya kompyuta, na hivyo kusababisha uharibifu wa taarifa na vifaa vya kielektroni.
4. Matumizi ya kupindukia (Addiction):

Fursa mbalimbali zinazopatikana mtandaoni kama vile michezo ya kompyuta, mitandao ya kijamii, katuni na muziki huwavutia sana watoto ambapo baada ya muda huwafanya watoto kuwa watumwa wa mtandao.Changamoto hizi zinaweza kupelekea kushuka kwa maendeleo ya watoto kitaaluma na kupata athari nyingine za kisaikolojia kama vile kuwa na msongo wa mawazo n.k
Angalizo kwa Watoto

Usitumie mitandao bila idhini ya wazazi au walezi.
Epuka kuwasiliana na watu usiowafahamu mtandaoni.
Usichapishe taarifa binafsi kuhusu wewe, mzazi au mlezi wako kama vile tarehe ya kuzaliwa, anwani ya makazi, nywila (password).
Epuka kutoa au kuchapisha taarifa hatarishi kama vile picha au video za utupu, vurugu au vitisho.
Usichapishe chochote kuhusu watu wengine bila ridhaa yao.
Elewa mipangilio na usome mikataba ya faragha kabla ya kutumia programu yoyote mtandaoni. Vinginevyo, unawe- za kuruhusu taarifa zako kuingiliwa au kuonwa na watu wengine pasipo wewe kujua.
Zuia (block) mtu yeyote anayetuma maoni ya kukusumbua, kukutishia au yasiyofaa kuhusu wewe na kuripoti kwa mtoa huduma wa programu husika au kituo cha polisi karibu nawe.
Chagua nywila (password) salama yenye tarakimu nane hadi kumi na mbili zenye mchanganyiko wa herufi, nambari na herufi za alama mfano “D0nt4g@t!” na uibadilishe mara kwa mara, angalau kila baada ya miezi mitatu (3). Kumbuka nywila (password) ni siri yako.
Tumia programu za kujikinga na virusi vya kompyuta na hakikisha programu hiyo inahuishwa mara kwa mara.