Kuanzia sasa, huduma, taarifa, na mawasiliano yote ya kiofisi yanayohusu TSV yatapatikana kupitia mifumo rasmi ifuatayo:
• Tovuti Rasmi: silicontz.org
• Barua Pepe (Emails): Wafanyakazi wote wanaohusika na TSV watatumia barua pepe rasmi zinazoishia na domain ya @silicontz.org (Mfano: jina@silicontz.org).
Tuna nasihi jamii na wadau wetu kuwa makini:
• Mawasiliano ya Kiofisi: MIA haitatambua barua pepe yoyote ya wafanyakazi wa TSV inayotoka kwenye akaunti binafsi za bure (kama vile @gmail.com, @yahoo.com, n.k.).
• Uthibitisho: Hakikisha kila unachoambiwa au maelekezo unayopewa yanatoka kwenye anuani yenye domain ya silicontz.org.
Tunamwomba kila mmoja azingatie mabadiliko haya ili kuepuka kuhadaika na matapeli mtandaoni.
Imetolewa na:
Uongozi, Moyo Islamic Academy (MIA).