Page 1 of 1

LEARN PHP PART THREE (ARRAYS II) - KISWAHILI

Posted: Sat Sep 26, 2026 6:16 pm
by songoroapps
Majibu ya challange kutoka katika sehemu iliyopita

1. echo $students[10];
2. $jina = students[2];
3. mohd

TUNAENDELEA
KUBADILISHA DATA KATIKA ARRAY.
Tuchukue array hii

Code: Select all

$matunda = ["embe","nanasi","machungwa"];
tunahitaji kubadilisha machungwa kuwa chungwa,
tunajua index ya machungwa ni 2, kuibadili tutaandika code kama ifuatavyo

Code: Select all

$matunda[2] = "chungwa";

KUENGEZA DATA KWENYE ARRAY
andika jina la array na wacha sehemu ya mabano ikiwa tupu

Code: Select all

$matunda[] = "papai";
print_r() METHOD

Tunatumia method ya print_r() kuangalia data zote zilizomo katika array yetu. print method hutumika wakati wa development na si kwa ajili ya presentation (final production)
Tutaitumia method hii katika kumalizia lesson hii pamoja na lesson nyengine zinazofuata

Code: Select all

print_r($matunda);
codes zetu kufikia hapa

Code: Select all

<?php
$matunda = ["embe","nanasi","machungwa"];
$matunda[2] = "chungwa";
$matunda[] = "papai";
print_r($matunda);
?>
matokeo yake

Image

KUFUTA DATA KWENYE ARRAY
tumia unset method kufuta data katika array

mfano

Code: Select all

unset($matunda[0]);
kama tuki print_r method array yetu tutapa

Array ( [1] => nanasi [2] => chungwa [3] => papai )

kwa vile tumefuta index 0.
tutapojaribu echo $matunda[0]; tutapata erro kwa vile tumefuta hiyo index pamoja na data zake,
Tunapofuta index moja, index nyengine hubakia kama zilivyo. Hivyo array yetu husebau index 0 kuwa undefined, hivyo index zilizobakia hubaki kama zilivyo.

TUTANEDELEA SEHEMU YA NNE.


CHALLANGE
soma array ifuatayo kisha jibu swali.

Code: Select all

$vyombo = ["dishi","kibakuli","kisahani","kijiko"];
SWALI:
andika variable ambapo variable hiyo itahifadhi na kuifuta $vyombo[0] (variable ihifadhi thamani ya $vyombo[0] na wakati huo huo iondoe $vyombo[0] kwenye array,)