CREATING TABLE - SQL WITH MYSQL WORKBENCH PART TWO- KISWAHILI
Posted: Sat Sep 26, 2026 5:19 pm
Data katika database ya sql inahifadhiwa katika jaduweli (table).
tutatumia database yetu ya school kutengeneza jaduweli la student.
kutengeneza jaduweli tunatumia key word
CREATE TABLE
ikifuatiwa na jina la la jaduweli tunalohitaji kutengeneza
kisha mabano, ndani ya mabano tunaweka taarifa tunazohitaji jaduweli letu kubeba.
Kwa mfano tunahitaji kutengeneza jaduweli linaloitwa students, ambalo litabeba nambari ya usajili ya mwanafunzi, jina lake kamili, na iwapo mwanafunzi anakaa hosteli au laa) tunaweza kuwa na table kama hivi.
SQL inahitaji kila data kuwa na aina yake ya data. katika sql tunazo aina tofauti za data ikiwemo
tinyint
int
bigint
varchar()
text
decimal
float
double
date
time
datetime
timestamp
bool/boolean
nk.
katika table yetu nambari ya usajili kwa sasa tuifanye kuwa int, jina kuwa ni varchar(), na iwapo anakaa hostel kuwa ni bolean. hivyo table yetu itakuwa kama hivi.
varchar() hubeba nambari ndani ya mabano.. hapa tumeruhusu jina kamili kuwa na hadi herufi 100 (tunataraji hakuna mwanafunzi ambae jina lake litazidi herufi 100)
kwa sasa hatuna taarifa yoyote katika kanzidata yetu. Unaweza kujaribu kuangalia table yake na data zake kwa kuandika
MATOKEO YAKE NI KAMA HAYA KATIKA PICHA

TUTAINGIZA DATA KUANZIA KATIKA MADA INAYOFUATA. ENDELEA KUFUATILI TANZANIA SILICON VALLEY
tutatumia database yetu ya school kutengeneza jaduweli la student.
kutengeneza jaduweli tunatumia key word
CREATE TABLE
ikifuatiwa na jina la la jaduweli tunalohitaji kutengeneza
kisha mabano, ndani ya mabano tunaweka taarifa tunazohitaji jaduweli letu kubeba.
Kwa mfano tunahitaji kutengeneza jaduweli linaloitwa students, ambalo litabeba nambari ya usajili ya mwanafunzi, jina lake kamili, na iwapo mwanafunzi anakaa hosteli au laa) tunaweza kuwa na table kama hivi.
Code: Select all
CREATE TABLE students(nambari_ya_usajili, jina_kamili,anakaa_hostel);
tinyint
int
bigint
varchar()
text
decimal
float
double
date
time
datetime
timestamp
bool/boolean
nk.
katika table yetu nambari ya usajili kwa sasa tuifanye kuwa int, jina kuwa ni varchar(), na iwapo anakaa hostel kuwa ni bolean. hivyo table yetu itakuwa kama hivi.
Code: Select all
CREATE TABLE students (nambari_ya_sajili INT, jina_kamili VARCHAR(100), anakaa_hostel BOOL);
kwa sasa hatuna taarifa yoyote katika kanzidata yetu. Unaweza kujaribu kuangalia table yake na data zake kwa kuandika
Code: Select all
SELECT * FROM students;