TANGAZO RASMI LA KOZI MPYA – FALL SEMESTER 2026 (In Shaa Allah)

Hedhi na nifasi
Haki za mwanamke
Maswali maalumu ya wanawake
Post Reply
User avatar
webmaster
Site Admin
Posts: 124
Joined: Mon Mar 23, 2026 11:03 am
Location: Pemba
Contact:

TANGAZO RASMI LA KOZI MPYA – FALL SEMESTER 2026 (In Shaa Allah)

Post by webmaster »

TANGAZO RASMI LA KOZI MPYA – FALL SEMESTER 2026 (In Shaa Allah)

Certificate in Islamic Sermon Delivery
Moyo Islamic Academy inayo furaha kutangaza kuanza kwa usajili wa kozi mpya ya Certificate in Islamic Sermon Delivery, itakayoanza katika Fall Semester 2026 (In Shaa Allah).
Kozi hii imebuniwa kwa lengo la kuwawezesha washiriki kupata maarifa, stadi na mbinu za kitaalamu za kuandaa na kuwasilisha khutba, mawaidha na mihadhara ya Kiislamu kwa ufasaha, hekima na ufanisi, kwa kuzingatia misingi ya Qur'an Tukufu na Sunnah, sambamba na mbinu za kisasa za mawasiliano.

Kozi hii inafaa kwa:
• Maimamu na Makhatibu.
• Walimu wa madrasa na taasisi za Kiislamu.
• Wanafunzi wa elimu ya Kiislamu.
• Wadau wa Da'wah.
• Kila Muislamu anayetamani kujenga uwezo wa kutoa khutba, mawaidha na mihadhara kwa umahiri na ufanisi.
Washiriki watanufaika kwa:
• Kujifunza misingi ya uandaaji wa khutba na mawaidha yenye ubora.
• Kuimarisha stadi za uwasilishaji na mawasiliano mbele ya hadhira.
• Kuelewa mbinu za kufikisha ujumbe wa Kiislamu kwa hekima na weledi.
• Kujenga kujiamini katika kutoa khutba na mihadhara kwa kuzingatia maadili na misingi ya Kiislamu.

Masomo yataanza: Fall Semester 2026 (In Shaa Allah).
Sifa za kujiunga, utaratibu wa maombi na maelezo zaidi yanapatikana kupitia:
https://www.moyoislamic.academy/home/ce/
FOMU INAPATIKANA HAPA: https://forms.gle/xs4EjuqA3yQQujfV6
Jisajili mapema na uwe sehemu ya kizazi cha walinganiaji wenye elimu, hikma na umahiri katika kuifikisha dini ya Allah kwa jamii.

"Moyo Islamic Academy – Educating the Ummah for a Better Tomorrow."
Post Reply

Return to “Wanawake katika Uislamu”

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 0 guests