Zanzibar kuanzisha mkakati wa "Halal Tourism” kukuza utalii

Post Reply
User avatar
webmaster
Site Admin
Posts: 124
Joined: Mon Mar 23, 2026 11:03 am
Location: Pemba
Contact:

Zanzibar kuanzisha mkakati wa "Halal Tourism” kukuza utalii

Post by webmaster »

Katika hatua yake ya kujiimarisha katika sekta ya utalii duniani, mamlaka ya Zanzibar imefungua milango mipya kwa kuanzisha kile kinachojulikana kama Utalii Halali, unaotajwa kuwa na mafungamano na historia ya kidini.

Utalii Halali ambao wanasema unafuata misingi ya haki na kutokuwa na mizengwe yoyote, unalenga kuwavutia watalii kutembelea visiwa hivyo na kuona maeneo ambayo historia yake ina uhusiano mkubwa na masuala ya kidini. Utalii kama huu umekuwa ukishuhudiwa katika maeneo mbalimbali duniani ikiwamo huko Jerusalem, Vatican, Morocco na hata Uturuki ambako watalii hutembelea na kujionea masuala yenye kukumbusha matukio na historia za kidini.

Utalii ni moja ya nguzo muhimu katika uchumi wa Zanzibar na sehemu kubwa ya mapato yake yanatokana na sekta hii yenye historia kubwa. Kwa mujibu wa takwimu kutoka kwa mamlaka zinazohusika na sekta hiyo, mnamo mwaka 2025 pekee, visiwa hivi vilipokea zaidi ya watalii laki 9. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka katika miaka ijayo kutokana na mipango inayolenga kuboresha na kutanua miundombinu ya usafiri.

Wakazi wengi visiwani humo wanaona kwamba kuwepo kwa mazingira rafiki pamoja na utulivu wa kimazingira ni moja ya sababu inayoendelea kuwavutia wageni wengi kutembelea visiwa vya Zanzibar.

"Kuhamasisha kwamba Wazanzibar wamejawa na upendo kila watalii wanavyoona upendo ambao Zanzibar tunao, namna ya kujumuika kwa pamoja wa hali ya nchini hali ya juu maana kila mtalii anahamasika kuja kuona upendo ambao tunao katika kisiwa chetu cha Zanzibar kwa hiyo Zanzibra ni nche yenye amani kwa hiyo watalii wanavutika kulingana na tunavyoishi."
Post Reply

Return to “General discussion (off-topic)”

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 0 guests