INSERTING AND READING DATA - SQL WITH MYSQL WORKBENCH PART THREE - KISWAHILI

APIs, Databases (MySQL, PostgreSQL)
Post Reply
User avatar
songoroapps
Posts: 6
Joined: Thu Mar 26, 2026 5:56 pm
Location: Mugumu, Serengeti, Tanzania
Contact:

INSERTING AND READING DATA - SQL WITH MYSQL WORKBENCH PART THREE - KISWAHILI

Post by songoroapps »

Karibu sehemu ya tatu.

Utakumbuka vyema kwenye kurasa iliyopita tulitengeneza table students, kwenye database ya school.
Structure ya table tuliyotengeneza ni muhimu kuielewa kwa ajili ya kuingiza data.
tunaweza kusahau structure ya table mara nyingi, hasa pale tunapokuwa na table nyingi ama tunapofanyia kazi database zaidi ya moja.

Kujikumbusha structure ya table andika DESCRIBE au DESC ikifuatiliwa na jina la table huska. na kwa table yetu itakuwa

Code: Select all

DESCRIBE students;
na matokeo yake ni hivi yanavyooneka katika picha hapo chini.

Image

field ndio jina la column, tuko na column tatu nambari_ya_sajili, jina_kamili, na anakaa_hostel. Type ni aina data. Tutaona Null, Key, Defautl na Extra katika masomo yafuatayo.
(note_ nambari ya usajili nimeandika nambari_ya_sajili - tutaacha kama ilivyo kwa sasa)

KUINGIZA DATA KWENYE TABLE

Tunaweza kuingiza data kwa syntax kama ifuatayo

Code: Select all

INSERT INTO jina_la_table(column1, column2, column3)
VALUES (value1, value2, value3);
mfano

Code: Select all

INSERT INTO students (nambari_ya_sajili, jina_kamili, anakaa_hostel)
VALUES (1, "Mustafa Khamis Ali", true);
baada ya kuingiza data andika

Code: Select all

SELECT * FROM students;
utaona orodha ya wanafunzi waliomo katika table yako. Boolean katika database inaweza kuhifadhiwa kama 1 kwa true na 0 kwa false

Pia tunaweza kuingiza values nyingi kwa wakati mmoja kama inavyoonekana katika mfano hapa chini.

Code: Select all

INSERT INTO students (nambari_ya_sajili, jina_kamili, anakaa_hostel)
VALUES 
(2, "Hadia Muhammed Khamis", false), 
(3,"Salma Suleiman Ali",true),
(4,"Mussa Omar Hamad", false),
(5, "Kassim Ali Kassim",true);
Pia unaweza kutumia njia ifuatayo iwapo unaingiza taarifa katika kila column ya database yako kwa mpangilio wake

Code: Select all

INSERT INTO students
VALUES (6, "Hasina Bakari Ali", false)
(Inawezekana kama umejaribu kuexcute sql query zaidi ya mara moja, data moja itaingia zaidi ya mara moja. Tutashughulikia hilo baadae).

KUSOMA DATA KUTOKA KATIKA TABLE.
Tunatumia SELECT kusoma data kutoka katika database yetu.
Teari ulishatumia hapo kabla SELECT * FROM.

Code: Select all

SELECT * FROM students;
Hii tunaisoma kama select all from students, kwa maana ya kwamba soma vyote kutoka table.

tunaweza kuondoa * na kuweka jina la column tunayohitaji kama vile

Code: Select all

SELECT jina_kamili FROM students;
kwa mujibu wa data zetu tutapa

Image

Pia tunaweza kutumia column zaidi ya moja kwa kuzitofautisha kutumi koma.

Code: Select all

SELECT jina_kamili, anakaa_hostel FROM students;
MATOKEO YAKE NI KAMA IFUATAVYO

Image


Itaendelea sehemu inayofuata
Attachments
Screenshot 2026-09-27 181300.png
Screenshot 2026-09-27 180609.png
Screenshot 2026-09-27 171308.png
Post Reply

Return to “Backend Development”

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 0 guests