1. echo $students[10];
2. $jina = students[2];
3. mohd
TUNAENDELEA
KUBADILISHA DATA KATIKA ARRAY.
Tuchukue array hii
Code: Select all
$matunda = ["embe","nanasi","machungwa"];
tunajua index ya machungwa ni 2, kuibadili tutaandika code kama ifuatavyo
Code: Select all
$matunda[2] = "chungwa";
KUENGEZA DATA KWENYE ARRAY
andika jina la array na wacha sehemu ya mabano ikiwa tupu
Code: Select all
$matunda[] = "papai";Tunatumia method ya print_r() kuangalia data zote zilizomo katika array yetu. print method hutumika wakati wa development na si kwa ajili ya presentation (final production)
Tutaitumia method hii katika kumalizia lesson hii pamoja na lesson nyengine zinazofuata
Code: Select all
print_r($matunda);
Code: Select all
<?php
$matunda = ["embe","nanasi","machungwa"];
$matunda[2] = "chungwa";
$matunda[] = "papai";
print_r($matunda);
?>
KUFUTA DATA KWENYE ARRAY
tumia unset method kufuta data katika array
mfano
Code: Select all
unset($matunda[0]);
Array ( [1] => nanasi [2] => chungwa [3] => papai )
kwa vile tumefuta index 0.
tutapojaribu echo $matunda[0]; tutapata erro kwa vile tumefuta hiyo index pamoja na data zake,
Tunapofuta index moja, index nyengine hubakia kama zilivyo. Hivyo array yetu husebau index 0 kuwa undefined, hivyo index zilizobakia hubaki kama zilivyo.
TUTANEDELEA SEHEMU YA NNE.
CHALLANGE
soma array ifuatayo kisha jibu swali.
Code: Select all
$vyombo = ["dishi","kibakuli","kisahani","kijiko"];
andika variable ambapo variable hiyo itahifadhi na kuifuta $vyombo[0] (variable ihifadhi thamani ya $vyombo[0] na wakati huo huo iondoe $vyombo[0] kwenye array,)