Code: Select all
$tunda1 = "embe";
$tunda2 = "tufaa";
$tunda3 = "pera";
$tunda4 = "chenza";
$tunda4 = "nanasi";
Code: Select all
$matunda= ["embe","tufaa","pera","chenza","nanasi"];
hii inatupa mpangilio mzuri wa kodi zetu, pia inarahisisha wakati wa kuita data kama ambavyo tutaona hapo baadae.
kuna njia mbili za kutengeneza array
ya kwanza, ambayo ni ya kisasa ni kama ambayo tumeitumia hapo juu.
Code: Select all
$arrayname = [data1,data2,data3,...];
Kuhusu matumizi ya tunapokuwa na maandishi, maandishi yanakuwa yanafungwa ndani ya double quotation " na ", ama hata quotation ya appostrophe inakubalika yaani ' na '. Nambari na kweli si kweli haziwekwi ndani ya alama hizo.
mfano
Code: Select all
$data = ["Police",112,'Fire', 113, true];
Njia nyengine tunayoweza kutumia kutengeneza array ni ya kizamani, na mfumo wake ni kama huu.
Code: Select all
$arrayname = array(data1, data2, data3,...);
KUSOMA TAARIFA ZA ARRAY
Aina ya array ambayo tumeisoma inaitwa indexed array. Tutaona aina nyengine hapo mbele.
Indexed array kila data hupewa nambari, kuanzia nambari 0. mfano
Code: Select all
$matunda= ["embe","tufaa","pera","chenza","nanasi"];
Hivyo tunapohitaji kwa mfano embe tunaenda kuliita kwa kutumia namba yake kama
Code: Select all
echo $matunda[0];
mfano
Code: Select all
<?php
$matunda= ["embe","tufaa","pera","chenza","nanasi"];
echo $matunda[0];
?>
embe
ITAENEDELEA SEHEMU INAYOFUATA (PART THEE)
MAZOEZI (MAJIBU YATATOLEWA PART THREE). Andika jibu lako katika comment (reply)
Soma kodi zifuatazo kisha jibu maswali
Code: Select all
<?php
$students = ["ali","mohammed","juma","ishaka","suleiman","mohd","joseph","salha","mariam","Said Juma Said"];
?>
1. Andika code za kuonesha "Said Juma Said";
2. Andika variable itakayohifadhi jina "juma", jina litoke kutoka katika array;
3. je tutapata nini tutakapoandika echo $students[5];