Tuchukue mfano wa kawaida. Rafiki yako akikuuliza, “Unaenda wapi?”, unaweza kumjibu, “Ninaenda Chake Chake.” Si lazima umwambie, “Ninaenda -5.2459, 39.7666,” ambazo ni coordinates (latitude na longitude) zinazotumika kwa eneo la Chake Chake kwenye ramani. Jina Chake Chake ni rahisi zaidi kulikumbuka na kulitumia kuliko coordinates zake.
Bai ndivyo ilivyo kwa variable. Data inapohifadhiwa katika memory, memory inakuwa na address yake, kwa mfano 0x7ffd1234. Tuchukulie kuwa katika address hiyo kuna nambari 16 kama thamani. Badala kutumia 0x7ffd1234 kila tunapohitaji nambari hiyo, tunatumia jina ambalo ni rahisi kulikumbuka.
Variable kwenye php huanza na $ na kufuatiwa na jina (variable name) kwa mfano $variable = value;
Code: Select all
$jina= "Musa Ali";
$umri= 12;
$amemalizaKusoma = false;
AINA ZA DATA ZA VARIABLE
1.Maandishi (String)
Code: Select all
$name = "Ali Musa Ali";Code: Select all
$age = 23;Code: Select all
$gpa = 4.5;Code: Select all
$isStudent = true;
$isDead = false;huhifadhi data nyingi katika variable moja
Code: Select all
$course = ["English","Math", "Biology"];Tunaweza kuonesha data za variable kwa kutumia neno "echo" kwa sasa.
mfano
Code: Select all
<?php
$schoolName = "Moyo Islamic Academy";
$studentName = "Yahya Muhammed Khamis";
$currentClass = 5;
echo "School name: $schoolName";
echo "Student name: $studentName";
echo "Class: Standard $currentClass";
?>
Matokeo ya program hii ni:-
Maandishi yote yamekaa kwenye mstari mmoja. Tabia ambayo sisi hatuitaki. Tunaweza kuengeza <br> katika kila echo kabla ya " ya kufungia.
Code: Select all
<?php
$schoolName = "Moyo Islamic Academy";
$studentName = "Yahya Muhammed Khamis";
$currentClass = 5;
echo "School name: $schoolName <br>";
echo "Student name: $studentName <br>";
echo "Class: Standard $currentClass <br>";
?>AHSANTE SANA. ITAENDELEA SEHEMU YA PILI