Shirika la Polisi wa Kimataifa (INTERPOL) limefanikiwa kuwakamata watu 201 wanaohusishwa na uhalifu wa mtandao katika operesheni maalum iliyopewa jina la “Operation Ramz,” iliyofanyika katika nchi 13 za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (MENA).
Operesheni hiyo, iliyodumu kuanzia Oktoba 2025 hadi Februari 2026, imelenga kuvunja mitandao ya ulaghai wa mtandao, mashambulizi ya phishing, usambazaji wa malware na utapeli wa kifedha uliokuwa ukiathiri maelfu ya watu katika ukanda huo.
Kwa mujibu wa INTERPOL, nchi zilizoshiriki operesheni hiyo ni pamoja na Algeria, Bahrain, Misri, Iraq, Jordan, Lebanon, Libya, Morocco, Oman, Palestina, Qatar, Tunisia na Falme za Kiarabu (UAE).
Shirika hilo limesema operesheni hiyo ndiyo ya kwanza ya aina yake kufanyika kwa kiwango kikubwa katika eneo la MENA kwa ushirikiano wa moja kwa moja kati ya vyombo vya usalama vya nchi mbalimbali.
Mbali na watu 201 waliokamatwa, mamlaka zimeeleza kuwa:
Washukiwa wengine 382 walitambuliwa
Waathirika 3,867 walibainishwa
Server 53 zilizokuwa zikitumika kuendesha mashambulizi ya mtandao zilitaifishwa
Maelfu ya taarifa za kiintelijensia zilikusanywa kusaidia uchunguzi zaidi
Ripoti zinaonyesha kuwa wahalifu hao walikuwa wakitumia mbinu mbalimbali za mtandao kuiba fedha na taarifa binafsi za watu kupitia:
Tovuti bandia za uwekezaji
Barua pepe za ulaghai (phishing)
Malware za kuiba taarifa
Mitandao ya “Phishing-as-a-Service” inayouza huduma za ulaghai mtandaoni
Nchini Algeria, polisi walifanikiwa kuvunja mtandao wa “Phishing-as-a-Service” baada ya kukamata vifaa vya kompyuta, simu na hard disk zilizokuwa na programu za ulaghai.
Katika moja ya matukio yaliyovuta hisia zaidi, polisi nchini Jordan walivamia eneo lililotumika kuendesha ulaghai wa kifedha kupitia jukwaa la uwekezaji bandia.
Hata hivyo, uchunguzi ulibaini kuwa watu 15 waliokuwa wakifanya kazi hiyo walikuwa waathirika wa biashara haramu ya binadamu. Walidaiwa kupelekwa Jordan kwa ahadi za ajira kutoka nchi za Asia, kabla ya pasipoti zao kuchukuliwa na kulazimishwa kufanya utapeli wa mtandao. Watu wawili wanaodaiwa kuongoza mtandao huo walikamatwa.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uhalifu wa Mtandao wa INTERPOL, Neal Jetton, amesema operesheni hiyo imeonyesha umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na wahalifu wa mtandao wanaovuka mipaka ya nchi.
Kwa mujibu wake, wahalifu wa mtandao wanaendelea kutumia teknolojia kufanya mashambulizi ya kimataifa, hivyo ushirikiano wa nchi mbalimbali ni muhimu ili kuwadhibiti.
Wataalamu wa usalama wa mtandao wanaonya kuwa ongezeko la mashambulizi ya phishing, ulaghai wa kifedha na matumizi ya malware linaendelea kuathiri serikali, taasisi za kifedha na wananchi wa kawaida duniani.
Makampuni ya usalama wa mtandao yaliyosaidia operesheni hiyo ni pamoja na Group-IB, Kaspersky, Trend Micro na Team Cymru.
CHANZO: The Hacker News
INTERPOL Yakamata Wahalifu 201 wa Mtandao katika Operesheni Kubwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini
- webmaster
- Site Admin
- Posts: 124
- Joined: Mon Mar 23, 2026 11:03 am
- Location: Pemba
- Contact:
Who is online
Users browsing this forum: No registered users and 0 guests