*Important Update*
YAHUSU: *Kughairishwa kwa Mitihani ya nusu muhula [Spring 2026] na Ugawaji upya wa alama kwa wanafunzi wetu wa IOU*
*Walengwa*: Programu zote za Shahada, Shahada ya Uzamili, Stashahada na Cheti cha Juu, *ISIPOKUWA* kozi zinazotegemea utafiti bila mitihani ya katikati ya muhula *yaani Research paper Based programs.
Assalamu alaikum wa rahmatullahi wa barakatuhu,
Ndugu Wanafunzi,
Tunatumai nyote ni wazima wa afya njema na mwenye nguvu, in sha Allah.
Tafadhali fahamu kuwa Mitihani ya nusu muhula ya muhula wa Spring 2026 *imeghairishwa* kwa sababu ya *changamoto zinaoendelea ulimwenguni* yaani vita vya mashariki ya kati na kupelekea kuwa na hali hatarishi kwa wanafunzi wetu kwa baadhi ya nchi kama vile Iran, Qatar, Oman, Saudi Arabia n.k. Ghairisho hili litahusu kwa mitihani ya nusu muhula iliyoratibiwa kuanza *tarehe 08 Mei 2026*, na mitihani ya ziada ya muhula iliyopangwa kuanza *Juni 16, 2026*.
Marks zilizotengwa kwa mitihani ya nusu muhula zitagawanywa upya kati ya mitihani ya mwisho yaani *final exams* na kwenye *assignments*. Maelezo ni kama ifuatavyo:
Muundo wa Tathmini Uliorekebishwa:
20% za marks za Midterms zitaongezwa kwenye *final exams*
10% za marks za Midterms zitaongezwa kwenye *assignments*
*ZINGATIA*:
1. Pre-midterm quizzes and module tests *lazima yakamilishwe kama ilivyoratibiwa*
2. Taarifa hii inahusu tu kwa kozi ambazo zinajumuisha midterm examinations (both revised and ongoing programs)
3. Kozi zilizotathminiwa kupitia karatasi za utafiti au vipengele visivyo vya mtihani yaani *research papers or non-exam components* hubakia vile vile bila kubadilika.
4. Wanafunzi wanashauriwa kuendelea na masomo yao mara kwa mara na kukaa sawa na shughuli za masomo.
Tunathamini uelewa wako na ushirikiano wako katika kipindi hiki.
Barak Allahu feekum.
*IMETOLEWA NA*:
Student Affairs Office (SAO)
International Open University – IOU
Monday, 20 April 2026, 3:42 PM
Kughairishwa kwa Mitihani ya nusu muhula [Spring 2026] na Ugawaji upya wa alama kwa wanafunzi wetu wa IOU
- webmaster
- Site Admin
- Posts: 124
- Joined: Mon Mar 23, 2026 11:03 am
- Location: Pemba
- Contact:
-
sharif.makame
- Posts: 8
- Joined: Sun Apr 12, 2026 11:30 am
- Contact:
Re: Kughairishwa kwa Mitihani ya nusu muhula [Spring 2026] na Ugawaji upya wa alama kwa wanafunzi wetu wa IOU
Tumepokea kwa huzuni maana kinachoendelea mashariki ni hatari kweli
Who is online
Users browsing this forum: No registered users and 0 guests