MUONGOZO JINSI YA KUINGIA KWENYE AKAUNTI YAKO

Post Reply
User avatar
webmaster
Site Admin
Posts: 124
Joined: Mon Mar 23, 2026 11:03 am
Location: Pemba
Contact:

MUONGOZO JINSI YA KUINGIA KWENYE AKAUNTI YAKO

Post by webmaster »

UTANGULIZI:
Hati hii imeandaliwa na Ofisi ya Huduma kwa Wanafunzi – MIA maalum kwa wanafunzi wetu wapya wanaosoma Chuo kikuu Huria cha Kimataifa – IOU ambao wanazungumza lugha ya Kiswahili ili iwe msaada na muongozo jinsi ya kuingia kwenye akaunti zao kwa ajili ya kusoma yaani DEGREE CAMPUS
Ndani ya hati hii, itatoa muongozo wa hatua kwa hatua jinsi ya kuingia kwenye akaunti na mambo muhimu ya kuzingatia.

1. Fungua Kivinjari “Web Browser”
Iwe unatumia simu janja au kompyuta mpakato n.k, kwa kawaida kunakuwa na “Web Browser” mbali mbali ambazo unaweza kutumia ili kuingia kwenye mtandao. Kwa mfano Mozilla Firefox, Microsoft Edge (zamani ikijulikana kama Internet Explorer), Chrome, Opera, Safari, Brave n.k


2. Fungua anuani husika
Mara baada ya kufungua “Web Browser” aanza kuandika anuani husika katika sehemu ya kuandikia anuani kama inavyoonekana hapo chini (taz. Mshale):-
Anuani ni campus.iou.edu.gm

3. Ingiza taarifa zako ili uweze kuingia kwenye akaunti yako.
Hapa utatakiwa kuingiza “username” na “Password” yako kisha bofya kitufe cha “Login”


4. Anza kufurahia usomaji kwa njia ya elimu masafa

Ukiweza kufungua ukurasa wa akaunti yako kama inavyoonekana hapo chini. Bila shaka utakuwa umefanikiwa kufungua akaunti yako. Na iwapo kama kutakuwa na changamoto. Basi hakiki “username and password” yako kwa usahihi. Kupata msaada zaidi usisite kuwasiliana nasi.



TIP 1: Tunza username na password yako
Ukiwa unatumia “computer” ya chuo, ofisini au umeazima sehemu. Jitahidi usiihifadhi username na password.
Labda iwe ni computer yako binafsi ambayo unatumia wewe pekee yako. Vile vile usimpe mtu usiemuamini password yako.
Kupata ushauri juu ya utunzaji wa password, usisite kuwasiliana nasi.
Tumegundua wanafunzi walio wengi wana tabia ya “Kusave Password” hasa wakiwa wanatumia computer za chuo au hata za maofisini. Hali ambayo inapelekea ukifungua “sub-domain” ya chuo tu inafunguka moja kwa moja.
Ili kuepukana na hili, ukiingia kwenye computer ambayo si yako na kukitokea kibox chenye maelezo ya Save na Not Now basi bofya sehemu ya “NOT NOW” kama inavyoonekana hapa chini.

TIP 2: UKIMALIZA USISAHAU KUFUNGA AKAUNTI YAKO
Iwe unatumia kifaa cha chuoni, ofisini, umeazima au chako binafsi, tunakuhimiza usisahau kutoka kwenye akaunti yako kwa kubofya “logout” kama alama ya mshale inavyoonesha hapo chini.


TIP 3 KWA MSAADA ZAIDI WASILIANA NASI
Ikiwa unapitia changamoto yoyote wasiliana nasi kwa anuani zifuatazo au kwa kupitia WhatsApp Group Chat zetu


Afisa Huduma kwa Wanafunzi,
Ofisi ya Huduma kwa Wanafunzi.
Ofisi: +255 743 328272 (WhatsApp Only)
Binafsi: +255 717 490671
Barua pepe: sso@moyoislamic.academy



Kwa wanafunzi wanawake
Afisa Huduma kwa Wanafunzi Wanawake,
Ofisi ya Huduma kwa Wanafunzi.

Ofisi: +255 755 875308 (WhatsApp Only)
Barua pepe: fsso@moyoislamic.academy

KWA HUDUMA ZAIDI
Ofisi ya Raisi na Uhusiano wa Kimataifa,

Ofisi: +255 766 061270 (WhatsApp Only)

Barua pepe: IRO@moyoislamic.academy & pemba@iou.edu.gm
Post Reply

Return to “IOU Campus”

Who is online

Users browsing this forum: No registered users and 0 guests